Muda mfupi ujao kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne ukilinganisha na kile kilichocheza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Robertinho amewaanzisha Fabrice Ngoma, Luis Miquissone, Said Ntibazonkiza na Jean Baleke kuchukua nafasi za Sadio Kanoute, Kibu Denis, Willy Onana na Moses Phiri.
Kikosi Kamili kilivyopangwa:
Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Henock Inonga (29), Fabrice Ngoma (6), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Said Ntibazonkiza (10), Luis Miquissone (11).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Sadio Kanoute (8), Kibu Denis (38), Willy Onana (7), John Bocco (22), Shaban Chilunda (27), Mohamed Mussa (14).