Leo saa 10 Simba Queens itashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL).
Miongoni mwa mabadiliko aliyofanya kocha Yussif Basigi kuelekea mchezo wa leo ni kumuanzisha mlinda mlango Wilfrida Seda akichukua nafasi ya mzoefu Janeth Shija.
Kikosi kamili kilichopangwa:
Wilfrida Seda (40), Fatuma Issa (5), Wincate Kaari (29), Violeth Nicholaus (26), Ruth Ingosi (20), Esther Mayala (23), Asha Djafari (24), Vivian Corazone (17), Jentrix Shikangwa (25), Aisha Juma (10), Precious Christopher (8).
Wachezaji wa Akiba:
Janeth Shija (30), Dotto Evarist (2), Emeliana Isaya (15), Jackline Albert (16), Janeth Nyagali (12), Ritticia Nabbosa (27), Elizabeth Wambui (4), Shelda Boniface (9), Asha Rashid (14).