Kauli ya Pablo baada ya ushindi dhidi ya Ruvu

Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Kocha Mkuu Pablo Franco ameweka wazi kuwa pointi tatu tulizopata ni muhimu na zitaongeza hali ya kujiamini kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Pablo amesema timu ilicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na kupata mabao matatu ambapo pia tulitengeza nafasi nyingi ambazo zingetufanya kupata ushindi mnono zaidi.

Pablo ameongeza kuwa Simba ni timu kubwa na inastahili kupata zaidi ya tulichokipata leo hivyo tutaendelea kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili kuwa imara.

“Ni ushindi muhimu tumepata, nilizungumza na wachezaji kuhusu hili, tunajua utaongeza morali kuelekea mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows.

“Tulicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza lakini tunastahili kupata zaidi, Simba ni timu kubwa na tunahitaji kurudi kwenye ubora wetu hivyo tunapaswa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza,” amesema Kocha Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER