Kauli ya Matola kuelekea mchezo na Ruvu Shooting

Kocha Msaidizi Seleman Matola, amesema mechi ya kesho dhidi ya Ruvu Shooting itakuwa ngumu lakini tumejiandaa kushinda na kuondoka na alama zote tatu.

Matola amesema wachezaji wote waliopo hapa jijini Mwanza wapo kwenye hali nzuri na tayari kwa kupambania alama hizo tatu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha huyo ameongeza kuwa lengo ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu hivyo tunapaswa kushinda kila mchezo ukiwemo huo wa kesho.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika wachezaji wote waliopo huku wapo tayari kwa mechi. Tunajua haitakuwa mechi rahisi kwani ligi inaelekea ukingoni kila timu inataka kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri lakini tupo tayari kupambana na kutetea ubingwa,” amesema Matola.

Kwa upande wake Nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mechi ya kesho ni mpya na wameachana na kumbukumbu ya mchezo uliopita na tupo tayari kupambana kulipa kisasi.

“Tunakumbuka tulipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu lakini mechi ya kesho ni mpya na kuna dakika 90 za kucheza, tupo tayari kupambana na tunaamini tutashinda,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER