Kaimu Kocha Mkuu, Hitimana Thierry amesema tutatumia mapumziko ya wiki mbili ya kupisha mechi za Kimataifa kuendelea kuimarisha kikosi chetu ili kurejesha makali yetu.
Hitimana amesema kikosi chetu kinapitia kipindi kigumu na wachezaji wanacheza kwa presha kutokana na matokeo mabaya tuliyopata mechi zetu za nyuma lakini kipindi hiki cha mapumziko tutajitahidi kuwaweka sawa wachezaji.
Hitimana ameongeza kuwa timu inacheza vizuri inatengeneza nafasi lakini inashindwa kuzitumia kutokana na wachezaji kuwa na presha hivyo kila kitu kitakaa sawa baada ya ligi kurejea.
“Ligi inasimama na tutakuwa na mapumziko ya wiki mbili, tutaitumia kuendelea kukiweka sawa kikosi kabla ya kurejea. Tuna idadi kubwa ya wachezaji majeruhi wengine watakuwa wamerejea kabla ya ligi.
“Tunajua tuna idadi kubwa ya wachezaji ambao wataenda kwenye timu zao za taifa lakini watakaobaki tutakuwa nao mazoezini ili kuendelea kuwaweka sawa tuna imani tutarudi katika ubora wetu,” amesema Hitimana.
One Response