Kauli ya Kocha Hitimana baada ya matokeo ya jana

Kocha msaidizi Hitimana Thierry ameweka wazi kuwa tulipaswa kumaliza mchezo wa jana kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Hitimana amesema nafasi tulizopata kama tungezitumia tungewapa mlima mkubwa wa kupanda Jwnaneng Galaxy lakini hatupaswi kulaumiana badala yake kusonga mbele.

Hitimana ameongeza kuwa kipindi cha pili wapinzani walirudi kwa kasi na kufanikiwa kutumia nafasi walizopata na kufuzu hatua ya makundi na hilo ni funzo kwetu.

“Tulitakiwa kumaliza mchezo kipindi cha kwanza, tulitengeneza nafasi za kufunga lakini hatukuweza wenzetu wamepata wamezitumia. Lakini huu ni mpira na tunapaswa kusonga mbele,” amesema Hitimana.

Hitimana amesema baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na kuangukia Kombe la Shirikisho Afrika tunapaswa kurudisha umoja ili kufanya vizuri hadi katika ligi ya nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER