Kauli ya Kocha Gomez baada ya Droo ya ASFC

Licha ya kuifunga Dodoma Jiji katika mechi zote mbili za Ligi Kuu msimu huu Kocha Didier Gomez amesema mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakuwa mgumu na tunapaswa kujipanga kuwakabili.

Droo ya michuano hiyo imepangwa leo Mei 11 ambapo tutacheza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Dodoma kati ya Mei 25, 26 au 27.

Kocha Gomez amesema kadri michuano inapozidi kusonga mbele ndiyo inazidi kuwa migumu ndiyo maana anaamini itakuwa mechi ngumu na tunapaswa kujipanga.

Gomez ameongeza kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunatetea ubingwa wa michuano hii kwani tuna timu bora na tunapaswa kudhihirisha hilo.

“Haitakuwa mechi rahisi kwetu dhidi ya Dodoma Jiji, tuliweza kuwafunga kwenye mechi mbili za ligi lakini haimaanishi hii itakuwa mechi nyepesi. Kwenye mashindano kadri yanavyozidi kupiga hatua ndiyo yanakuwa magumu,” amesema kocha Gomez.

Mshindi wa mchezo wetu atacheza hatua ya nusu fainali na mshindi kati ya Rhino Rangers dhidi ya Azam FC.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER