Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema maandalizi kuelekea mchezo wetu wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji yapo kwenye hatua nzuri.
Kocha Fadlu amesema baada ya mchezo uliopita dhidi ya Azam FC kikosi kilifanya mazoezi ya utimamu wa mwili jana na leo kimesafiri tayari kwa mchezo wa kesho.
Kocha Fadlu ameongeza kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunacheza vizuri na kupata ushindi huku tukihakikisha tunawadhibiti vizuri Dodoma Jiji.
“Maandalizi yamekamilika na tupo tayari kwa mchezo wa kesho, ratiba ni ngumu lakini tupo tayari na malengo yetu ni ushindi.”
“Kikosi kipo kwenye umbo zuri najivunia timu yangu kwa jinsi tunavyocheza,” amesema Kocha Fadlu.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, Kelvin Kijili amesema kwa upande wao wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ingawa amekiri utakuwa mgumu.
“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa na lengo likiwa ni kuchukua pointi zote tatu,” amesema Kijili.