Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema katika kipindi cha wiki nzima tangu kikosi kirejee kutoka Misri amekuwa akiwasisitiza wachezaji kwenye kufunga mabao ili kuweza kufanikiwa kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Fadlu amesema tunahitaji kufunga mabao matatu ili kuweza kufuzu nusu fainali lakini amewaandaa wachezaji kuhakikisha tunafunga zaidi ya mabao manne.
Fadlu ameongeza kuwa Simba ni Klabu kubwa Afrika na inataka mafanikio yakiwemo kutinga nusu fainali na ikishindikana atakuwa tayari kuwajibika.
“Tunahitaji mabao matatu ili kufuzu nusu fainali na hii wiki nzima tumefanya mazoezi walau tufunge mabao zaidi ya manne na sio matatu pekee,” amesema Fadlu.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anakuwa sehemu ya kikosi kilichoandika historia ya kuipeleka timu nusu fainali.
“Tukiwa na wachezaji wageni tunawaambia kuwa kufika robo fainali sio mafanikio kwakuwa sisi tushafanya mara nyingi ila wanatakiwa kuhakikisha tunasaidiana kutoka hapa na kuifikisha timu nusu fainali,” amesema Zimbwe Jr.