Kauli ya Kocha Fadlu kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Al Masry

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry yamekamilika na kikosi kipo kwenye hali nzuri.

Fadlu amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa uzoefu wa wapinzani lakini tumewaandaa wachezaji vyakutosha kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Fadlu ameongeza kuwa licha ya Al Masry kuwa na kocha mpya lakini bado wana kikosi imara ambacho kinaweza kuleta ushindani dhidi ya timu yoyote.

“Itakuwa mechi ngumu, lakini tumejiandaa vizuri. Kikosi chetu kimepata muda mzuri wa maandalizi na tumefanya mazoezi hapa Misri kwa siku nne na tupo tayari kwa mchezo,” amesema Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji, Steven Mukwala amesema wapo tayari kuhakikisha wanapigania nembo ya klabu.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kuhakikisha tunapambana kwa dakika zote 90 ili kuwapa furaha Wanasimba wote ambao tunaamini watakuwa nyuma yetu,” amesema Mukwala.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER