Kocha Mkuu Fadlu Davids ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani.
Kocha Fadlu amesema pamoja na CS Sfaxien kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi la kumfuta kazi kocha wao lakini bado wana timu imara ambayo inaundwa na vijana pamoja na wazoefu.
Akizungumzia kuhusu kikosi chetu, Fadlu amesema wapo kwenye hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa kesho huku malengo yakiwa kuhakikisha pointi tatu zinapatikana.
“Utakuwa mchezo mgumu, ikifika hatua hii kila mchezo unakuwa mgumu hasa ukiwa ugenini lakini tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo chanya,” amesema Kocha Fadlu.
Kwa upande wake mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa kupata ushindi kwenye mechi ya kesho ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.
“Tunajua tupo ugenini na haitakuwa mechi nyepesi lakini tumejiandaa vizuri na tupo tayari kwa Mapambano,” amesema Che Malone.
Mchezo wetu wa kesho utapigwa saa moja usiku kwa saa za Tanzania katika Uwanja wa Olympique De R – Tunis.