Kauli ya Kocha Basigi kuelekea mchezo dhidi ya JKT Queens

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Yussif Basigi amesema mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya JKT Queens ni muhimu kwakuwa utaamua hatima ya ubingwa.

Basigi amesema mshindi wa mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa 10 jioni atakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka bingwa msimu huu.

Basigi ameongeza kuwa mchezo dhidi ya JKT haujawahi kuwa mwepesi kutokana na ubora wa wapinzani lakini tupo tayari kuwakabili.

“Utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia unaamua ubingwa wa Ligi kutokana na nafasi za timu zote mbili lakini tumejipanga na tupo tayari kupambana kupata ushindi,” amesema Basigi.

Simba Queens ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi akiwa na pointi 37 alama moja nyuma ya JKT.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER