Kauli ya Fadlu kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya TMA

Kocha mkuu, Fadlu Davids amesema amewaandaa wachezaji kimwili na kiakili kuelekea mchezo wa hatua ya 32 bora ya CRDB Federation Cup dhidi ya TMA Stars utakaopigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.

Fadlu amesema aina hii ya michuano ni migumu kwakuwa unahitaji kushinda ili kufuzu hatua inayofuata na hakuna mechi ya kujiuliza ndio maana tumechukua tahadhari zote.

Fadlu amesema ameifuatilia TMA ni timu nzuri ina uwezo wa kufunga mabao pamoja na kuzuia hivyo ni lazima kuchukua tahadhari na kutumia vema nafasi zote tutakazozipata.

“Tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huu kwakuwa hatuna njia nyingine kama tunahitaji kufuzu hatua inayofuata.

“TMA ni timu nzuri inacheza soka safi kuanzia kwenye kuzuia mpaka kufunga kwahiyo tunahitaji kuchukua tahadhari ili kushinda,” amesema kocha Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema pamoja TMA kushiriki Championship hatutaidharau na mchezo wa kesho tutauchukulia kama mechi nyingine kubwa.

Salim amesema mara nyingi timu zinapokutana na Simba huwa zinajituma zaidi ya mara 10 lakini wachezaji wanalijua hilo na wapo tayari kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki wetu.

“Kwetu wachezaji kila mchezo tunaupa umuhimu mkubwa, tunajua itakuwa mechi ngumu kwakuwa TMA watakuja kwa kujituma lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kufuzu kwa hatua inayofuata,” amesema Ally.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER