Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba utakaopigwa kesho katika Uwanja wa KMC Complex utakuwa mgumu kutokana nafasi waliyopo wapinzani wetu.
Matola amesema Pamba haiko sehemu salama kwenye msimamo hivyo wanatumia nguvu kubwa katika kila mchezo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
Matola ameongeza kuwa pamoja na ugumu wa mchezo huo lakini tumejipanga vilivyo kuhakikisha tunapata matokeo chanya.
“Utakuwa mchezo mgumu kutokana nafasi waliyopo Pamba lakini Simba ni timu kubwa na inaweza kucheza kwenye mazingira yoyote kwa ajili ya kutafuta pointi tatu,” amesema Matola.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema wapo tayari kupambana hadi mwisho kuona alama tatu muhimu zinapatikana.
“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, Pamba ni timu bora na haipo kwenye nafasi nzuri lakini tumejipanga kupata pointi zote tatu,” amesema Ally.