Karibu Simba Mohamed Bajaber

Kiungo mshambuliaji, Mohamed Bajaber amejiunga na kikosi chetu kutoka Polisi Kenya kwa mkataba wa miaka mitatu.

Bajaber (22) raia wa Kenya ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na ana uwezo wa kucheza winga zote mbili pamoja na mshambuliaji namba 10.

Msimu uliopita akiwa na Polisi, Bajaber amefunga mabao 11 huku akisadia kupatikana kwa mengine manne na kuipa miamba hiyo ubingwa wa Ligi Kuu nchini Kenya.

Kabla ya kujiunga na kikosi chetu Bajaber alikuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ kinachojiandaa na michuano ya CHAN ambayo inaanza kutimua vumbi leo.

Bajaber ambaye mashabiki wa soka nchini Kenya wanamtambua kama ‘Star Boy’ ni miongoni mwa usajili tuliofanya kuelekea msimu mpya wa mashindano ambao tuna matarajio nao makubwa.

Star Boy ataungana na wachezaji wenzake kambini nchini Misri kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER