Karibu Simba Jonathan Sowah

Mshambuliaji, Jonathan Sowah atakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Sowah (26) raia wa Ghana tumemsajili kutoka Singida Black Stars tunaamini atakuwa na mchango mkubwa kikosini kutokana na uzoefu na ubora wake katika michuano ya ndani na kimataifa.

Sowah ni mshambuliaji ambaye anahitaji nafasi moja tu ili kuweka mpira kambani na hicho ni moja ya kitu ambacho kimetuvutia kuipata saini yake.

Msimu uliopita akiwa na Singida Black Stars, Sowah amefunga mabao 15 katika michezo 15 na hilo linaonyesha dhahiri uwezo alionao.

Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga nasi Sowah amesema “Simba ni timu kubwa na mara walivyonitafuta ilikuwa rahisi kwangu kukubaliana nao kwakuwa ni ndoto ya kila mchezaji kupata nafasi kama hii.”

“Malengo ya klabu yanaendana na malengo yangu binafsi, mimi ni mshambuliaji kazi yangu ni kufunga ili kuisadia timu kupata ushindi na ndicho kilichonileta Simba,” amesema Sowah.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER