Kiungo mkabaji, Hussein Daudi Semfuko atakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Semfuko (21) ni kijana wa kitanzania mwenye uwezo mkubwa uwanjani na ndicho kilichotuvutia na kumsajili kutoka Coastal Union ya Tanga.
Semfuko ni pendekezo la kocha Fadlu Davids ambaye anaamini uwezo wa kijana huyo utakuwa msaada mkubwa kwa timu yetu kwenye michuano mbalimbali.
Msimu uliopita akiwa Coastal Union, Semfuko alikuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza na kufanikiwa kufunga bao moja.
Malengo yetu msimu huu ni kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa ambao watakuwa na tija kwa timu na kukifanya kikosi chetu kuwa na uwiano sawa.