Kiungo mkabaji, Alassane Maodo Kante amejiunga na kikosi chetu kutoka CA Bizertin ya Tunisia kwa mkataba wa miaka miwili huku tukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja.
Kante (25) raia wa Senegal ni kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia huku sifa yake kubwa ikiwa kupiga pasi zinazofika kwa usahihi kwa walengwa iwe mbali au karibu.
Msimu uliopita Kante amefanikiwa kufunga mabao manne huku akisadia kupatikana kwa mengine nane (Assisti) akiwa muhimili mkubwa wa CA Bizertin.
Kante ni mmoja ya wachezaji ambao Uongozi wa klabu pamoja na benchi la ufundi lina matumaini nae makubwa katika michuano ya ndani na Kimataifa.
Kante anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa ndani ya kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa mashindano baada ya jana kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati, Rushine De Reuck.