Mlinzi wa kulia Shomari Kapombe, amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa mashabiki (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).
Kapombe amewapiku mlinzi wa kati Henock Inonga na winga Peter Banda ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Kapombe atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP ikiwa ni zawadi ya kuibuka kidedea.
Lengo la kuanziasha tuzo hizo ni kuongeza hali ya kujituma kwa wachezaji ili kuipigania zaidi timu kupata matokeo ya ushindi.
Mchanganuo wa kura ulivyokuwa
Shomari Kapombe kura 821 (67%)
Henock Inonga kura 277 (23%)
Peter Banda kura 125 (10%)
One Response