Mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema aina yake ya kushangilia baada ya kufunga bao la tatu ni ‘kuwazodoa’ waliokuwa wakishangilia jana kufuatia kuongoza ligi kwa saa 24.
Kapombe amesema alikuwa akiwauliza ‘kiko wapi’ baada ya kufunga bao hilo ambalo lilikata kabisa matumaini ya Tabora United ya kuambulia hata alama moja.
Kapombe alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti la chini chini la mguu wa kushoto akimalizia pasi safi iliyopigwa na Leonel Ateba.
“Nilikuwa nauliza ‘kiko wapi’ kwakuwa wengi walidhani tusingeweza kupata ushindi hasa baada ya Tabora kuzifunga timu kubwa kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi,” amesema Kapombe.