Kanoute arejea mazoezini, Sakho bado kidogo

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute, leo amerejea mazoezini baada ya kupona maumivu ya bega aliyopata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Septemba 25, mwaka huu.

Kanoute raia wa Mali amekosa mechi mbili za Ligi Kuu dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji kutokana na kuwa majeruhi.

Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho yeye ataendelea kukaa nje kwa wiki moja zaidi akiendelea kuuguza jeraha la enka chini ya uangalizi wa daktari alilopata katika mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji.

Baada ya mapumziko ya siku mbili kikosi leo kimeanza mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterans na wachezaji ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa.

Wachezaji wetu 16 wameitwa kwenye zao za taifa hivyo waliobaki wamechanganywa na timu ya vijana kufanya mazoezi ili walimu waendelee na programu yao.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER