Kagere kuongoza mashambulizi dhidi ya Namungo

Mshambuliaji Medie Kagere amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa nusu fainali ya michuano ya Mapinduzi dhidi ya Namungo utakaopigwa Uwanja wa Amani saa 2:15 usiku.

Kagere atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji, Kibu Denis, Rally Bwalya na Pape Ousmane Sakho.

Jonas Mkude na Sadio Kanoute wamepangwa katika idara ya kiungo ya ulinzi huku Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama mabeki wa kati.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomary Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Denis Kibu (38), Sadio Kanoute (3), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (17).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Israel Mwenda (5), Pascal Wawa (6), David Udoh (33), Bernard Morisson (3), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Hassan Dilunga (24).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER