Washambuliaji Medie Kagere na Kibu Denis wamepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa 10 jioni.
Kagere na Kibu watapata huduma ya karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Hassan Dilunga na Bernard Morrison.
Jonas Mkude na Mzamiru Yassin wamepangwa katika kiungo wa ulinzi huku Joash Onyango na Pascal Wawa wakicheza pamoja nafasi ya mabeki wa kati.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Jonas Mkude (20), Hassan Dilunga (24), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Kibu Denis (38), Bernard Morrison (3).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Sadio Kanoute (13), Duncan Nyoni (23), John Bocco (22), Pape Sakho (23), Yusufu Mhilu (27).