Mshambuliaji wa Simba Queens, Jentrix Shikangwa amechaguliwa mchezaji bora wa Ligi ya Wanawake Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) wa mwezi Machi.
Jentrix ambaye ni kinara wa ufungaji katika SLWPL amecheza dakika 270 mwezi Machi huku akifunga mabao matatu.
Jentrix raia wa Kenya amekuwa muhimili katika safu yetu ya ushambuliaji na mwiba mchungu kwa wapinzani wetu.
Jentrix anakuwa mchezaji wetu wa pili kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi baada ya aliyekuwa nahodha wetu Opa Clement kufanya hivyo Desemba kabla ya kutimka kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Uturuki katika klabu ya Besistas.