Iwe jua, iwe mvua tunahitaji ushindi kutinga robo fainali

Hakuna neno moja unaweza kuzungumzia mchezo wetu wa mwisho wa kundi D wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie utakaopigwa saa nne usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa zaidi ya kusema machozi, jasho na damu lakini lazima ushindi upatikane.

Leo ni mechi muhimu na tumeipa ukubwa kama fainali sababu tunahitaji ushindi ili tufuzu Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tuna bahati ya kucheza mchezo wetu wa mwisho ambao unaamua hatima yetu katika uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wetu ambao tunaamini watakuja kwa wingi kushudia tukisonga mbele.

Tunachoomba kwa sasa ni ushindi na lisitokee jambo katikati na kusababisha kushindwa kufikia malengo yetu ya kuingia robo fainali sababu hilo ndilo lengo kuu kuanzia kwa uongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki.

PABLO: TUMEPATA MAANDALIZI YAKUTOSHA

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema tulikuwa na wiki moja tulivu ya kufanya maandalizi na kitu kizuri hakuna mchezaji yeyote ambaye amepata majeraha.

Pablo amesema kila timu kwenye kundi letu ina nafasi ya kufuzu kama itashinda hivyo tunapaswa kuchukua tahadhari na kuhakikisha tunatumia vizuri nafasi tutakazopata katika uwanja wetu wa nyumbani.

“Kitu kuzuri ni kuwa tulipata muda mrefu wa kufanya maandalizi, wachezaji wako vizuri na hatuna presha. Kundi letu bado lipo wazi na kila timu ina nafasi ya kutinga robo fainali hivyo tutacheza kwa tahadhari,” amesema Pablo.

ZIMBWE JR ATOA NENO

Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo na wanajua Wanasimba wanahitaji furaha hivyo watahakikisha lengo linafikiwa.

“Kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huu, na huwa tunakumbushana mazoezini hata tukiwa kambini, tunamuomba Mwenyezi Mungu atujalie tushinde tuwape furaha Wanasimba na Watanzia wote kwa ujumla,” amesema Zimbwe Jr’.

HALI YA KIKOSI

Wachezaji wote wako katika hali nzuri morali ipo juu kila mmoja anatamani kuaminiwa na benchi la ufundi ili atuwakilishe katika mchezo wa leo.

Nyota wawili pekee ndiyo tutawakosa Hassan Dilunga ambaye ni majeruhi na Clatous Chama ambaye kanuni hazimruhusu kucheza mashindano haya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER