Uongozi wa klabu umetangaza viingilio vya mchezo wetu wa mwisho wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili Aprili 3, mwaka huu.
Lengo la kutangaza mapema viingilio ni kuepusha usumbufu kwa mashabiki watakaopata nafasi siku ya mchezo.
Viingilio hivyo vimepangwa kama ifuatavyo:
Mzunguko Sh 3,000
VIP C Sh 10,000
VIP B Sh 20,000
VIP A Sh 30,000
Tiketi zitaanza kuuzwa kesho kupitia mitandao ya simu ambapo vituo vitakavyotangazwa muda wowote kuanzia sasa.
One Response