Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa Jumapili, Novemba 5 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa
Ahmed amesema viingilio vimetangazwa wiki moja kabla ili kuwapa nafasi mashabiki kununua tiketi mapema kuepuka usumbufu.
Sisi ndio wenyeji wa mchezo na tayari tumeweka hadharani viingilio ambavyo ni rafiki ili kuwafanya mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Viingilio ni kama ifuatavyo:
Mzunguko Sh. 5,000
Vip A Sh. 40,000
Vip B Sh. 30,000
Vip C Sh. 20,000
Orange Sh. 10,000
Platinum Sh. 150,000
Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kupitia kwenye mitandao na vituo ambavyo zitaanza kuuzwa vitatangazwa muda wowote kutoka sasa.