Leo tumetangaza viingilio vya mchezo wetu wa fainali ya mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mei 25.
Tumeamua kutangaza viingilio mapema ili kuwapa nafasi mashabiki kukata tiketi mapema na kuondoa usumbufu usio wa lazima siku ya mchezo.
Maneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally, amesema dhumuni la kuweka hadharani viingilio mapema ni kuwapa nafasi mashabiki kujitokeza kwa wingi.
“Tumedhamiria kubeba ubingwa wa michuano hii, ndio maana tunahitaji sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wetu. Tunaamini furaha ya kila Mwanasimba ni kuiona timu yetu ikitwaa ubingwa wa Afrika kwahiyo tunahitaji kujitoa ili kufanikisha malengo haya,” amesema Ahmed.
Hivi hapa Viingilio vilivyotangazwa:
Mzunguko – Tsh. 7,000.
VIP C – Tsh. 20,000.
VIP B – Tsh. 30,000.
Platinum – Tsh. 250,000.