Tiketi za mchezo wetu wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravo FC kutoka Angola utakaopigwa Novemba 27 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.
Viingilio hivyo vimetangazwa mapema na pia ni rafiki kwakuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunaujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewaomba mashabiki wetu kununua tiketi mapema ili kupunguza usumbufu katika siku ya mchezo.
Ahmed ameongeza kuwa malengo ya klabu ni kuhakikisha tiketi zinamalizika siku mbili kabla ya mchezo.
“Viingilio tayari tumevitangaza na tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao, tunachowaomba Wanasimba ni kununua tiketi mapema ili kuujaza Uwanja mapema,” amesema Ahmed.
Hivi hapa Viingilio vya mchezo:
VIP A 50,000
VIP B 20,000
VIP C 15,000
Machungwa 10,000
Mzunguko 5,000