Hiki hapa kikosi kilichopangwa kuivaa Dar City Leo

Kocha Mkuu Pablo Franco amefanya mabadiliko kidogo ya kikosi kuelekea mchezo wetu wa hatua ya 32 ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Dar City utakaopigwa leo saa moja usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Pablo amefanya mabadiliko ya wachezaji sita ambao wameanza moja kwa moja katika mchezo wa leo ambao tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Mlinda mlango Beno Kakolanya ameanza langoni kuchukua nafasi ya Aishi Manula wakati walinzi wa pembeni Israel Patrick na Gadiel Michael wakichukua nafasi za Shomari Kapombe na Mohamed Hussein.

Kennedy Juma amechukua nafasi ya Joash Onyango katika beki wa kati huku Erasto Nyoni akipangwa kiungo wa ulinzi.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Hassan Dilunga (24), Clatous Chama (17), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Yusuf Mhilu (27).

Wachezaji wa akiba

Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Pascal Wawa (6), Mzamiru Yassin (19), Bernard Morrison (3), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Jimmyson Mwinuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER