Kikosi chetu leo saa 11 jioni kitasafiri kwa ndege kuelekea jijini Arusha kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa na Msimu Mpya wa Ligi 2021/22.
Kikosi kitakuwa na wachezaji 21 huku wale waliopo kwenye majukumu ya Timu ya Taifa (Taifa Stars) watajiunga na wenzao baadaye.
Kambi ya Arusha inakuwa ya pili baada ya ile ya siku 18 ya nchini Morocco.
Kikosi kitarejea jijini Dar es Salaam siku chache kabla ya kilele cha Simba Day, Septemba 19.
Kikosi Kamili kinachosafiri
Makipa
- Beno Kakolanya
- Ally Salim
- Ahmed Feruz
Mabeki
- Pascal Wawa
- Gadiel Michael
- Henock Baka
- Kennedy Juma
- Joash Onyango
Viungo
- Jonas Mkude
- Rally Bwalya
- Bernard Morrison
- Yussufu Mhilu
- Abdulsamad Kassim
14 Sadio Kanoute - Duncan Nyoni
- Jimmyson Mwanuke
- Hassan Dilunga
- Pape Sakho
Washambuliaji
- John Bocco
- Ibrahim Ajib
- Cris Mugalu