Kuelekea ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL) tumekuwa na utaratibu wa kufanya hamasa kwa ajili ya kuwafanya mashabiki wajitokeze kwa wingi na safari hii zitazinduliwa katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kufika Coco Beach tutaanza na maandamano ambapo magari magari zaidi ya 200 yatatoka Makao Makuu ya klabu Msimbazi kuelekea Coco.
Siku hiyo kutakuwa na michezo mbalimbali pamoja na burudani ambapo makundi na matawi yetu yatashiriki kama tulivyowahi kufanya miezi kadhaa iliyopita.
Hii hapa ratiba kamili ya hamasa.
Jumamosi Oktoba 14 – Uzinduzi wa Hamasa (Coco Beach)
Jumatatu Oktoba 16
kutakuwa na Operation ya kuweka bendera na kubandika picha (Paint the City) ambapo tutatembelea sehemu zenye mkusanyiko wa watu mbalimbali kama stendi, masoko n.k na kuweka picha za hamasa kuelekea AFL.
Jumanne Oktoba 17 Kispika Day
Tutazunguka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kuhamasisha ambapo tutaanzia Mbagala, Tabata, Mbezi Malamba Mawili na kumalizia Manzese Uwanja wa Fisi.
Jumatano Oktoba 18
Mkutano baina ya klabu, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Alhamisi Oktoba 19
Mkutano wa makocha na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wenyewe.