Zoezi la hamasa kuelekea mchezo wetu wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa imeingia siku ya pili na leo imefanyika kwenye Mabasi ya Mwendokasi.
Zoezi hilo limeanzia kituo cha Garezani Kariakoo hadi Mbezi Luis Stendi ya Magufuli ambapo zoezi la kuuza tiketi limeendelea kama kawaida.
Hamasa ya leo imefana kutokana na ushirikiano mkubwa tuliopata njiani tangu tunatoka Gerezani mpaka kufika Mbezi.
Meneja na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema zoezi la hamasa tumefanikiwa kwa asilimia kubwa kilichobaki ni mashabiki kuendelea kununua tiketi ili Jumamosi tuujaze uwanja.
Ahmed amesema kama mashabiki watajitokeza kwa wingi uwanjani Jumamosi hakuna namna Jwaneng Galaxy watatoka lazima tuwafanye kitu mbaya hivyo ni muda wa Wanasimba kuungana ili kufanikisha jambo hili.
“Tunawaomba mashabiki mje kwa wingi uwanjani Jumamosi, wale Jwaneng Galaxy hawawezi kutoka kwa namna yoyote.
“Tupo tayari kulipa kisasi, uwezo tunao timu tunayo kilichobaki mashabiki ni kujitokeza kwa wingi tukamilishe jambo letu la kutinga robo fainali,” amesema Ahmed.