Hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Bravo kuzinduliwa Jumapili

Zoezi la hamasa kuelekea mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Bravo Do Marquis kutoka Angola litazinduliwa Jumapili Novemba, 24 katika Tawi la Wekundu wa Msimbazi Bombambili kwa Chela lililopo Mombasa Madizini, Dar es Salaam.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kama ilivyo kawaida yetu kila unapofika muda wa kucheza mechi za Kimataifa huwa tunakuwa na hamasa na msimu huu tunazindua Mombasa Ukonga.

Ahmed amesema kabla ya uzinduzi huo kutatanguliwa na zoezi la kutoa msaada katika Kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa Orphanage Center kilichopo Mbweni lengo likiwa ni kurejesha kwa jamii zoezi litakalofanyika Jumamosi Novemba, 23.

“Jumatatu ya Novemba 25 tutakuwa na zoezi la kuchangia damu kwa Matawi, vikundi na mashabiki wote wa Simba nchi nzima lengo likiwa ni kuisaidia jamii ambayo ina uhitaji mkubwa wa damu,” amesema Ahmed.

Akizungumza kuhusu mchezo wenyewe Ahmed amesema “Bravo inatokea kwenye Taifa ambalo sio kubwa kimpira na kama mashabiki wetu watajitojeza kwa wingi wakiwa na jezi na kushangilia kwa nguvu hakuna namna wataepuka kipigo Novemba 27.”

Ahmed ameongeza kuwa “mara ya mwisho kushiriki Kombe la Shirikisho tuliishia robo fainali lakini sasa mipango ni kuvuka hatua hiyo na kinachotupa jeuri ni ubora wa kikosi tulichonacho.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER