Kocha Mkuu, Didier Gomez na kiungo wetu mshambuliaji Clatous Chama wameibuka kidedea kwenye tuzo za mwezi Aprili za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kocha Gomez ameshinda tuzo hiyo baada ya kutuwezesha kushinda mechi zote saba tulizocheza ndani ya Aprili sawa na asilimia 100.
Hii ni tuzo ya kwanza ya kocha bora wa mwezi wa Ligi kwa Gomez tangu alipojiunga nasi Februari mwaka huu.
Kwa upande wake Chama raia wa Zambia amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi huu kutokana na mchango mkubwa aliotoa kwa timu akifunga mabao matatu na kusaidia kupatikana kwa mengine matano (assist).
Tuzo hii imekuja siku moja baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki inayotolewa na Emirate Aluminium Profile (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month.
2 Responses
More congratulations to clatous chama the brain
Well deserved. 🦁