Kocha Mkuu Didier Gomes, ameshinda Tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu Msimu wa 2020/21 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) 2021.
Gomes amewashinda Francis Baraza wa Kagera Sugar na George Lwandamina wa Azam FC ambao aliingia nao kwenye fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Tuzo hiyo Gomes amekabidhiwa na Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kim Poulsen.