Gomes awamwagia sifa wachezaji mechi dhidi ya Azam

Kocha Mkuu Didier Gomes amewasifu wachezaji kwa kujitoa na kupambana hadi mwisho kwenye mchezo wa jana wa ligi kuu dhidi ya Azam FC.

Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na matumizi makubwa ya nguvu hasa kipindi cha kwanza tulisawazisha bao dakika ya 84 kupitia kwa Medie Kagere baada ya jitihada kubwa za wachezaji.

Gomes amesema wachezaji wengi walioanza kwenye mchezo wa jana hawakupata nafasi sana kwenye kikosi cha kwanza msimu huu lakini wamejitahidi kupambana na kujitoa muda wote uwanjani.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wangu walipambana muda wote, mechi ilikuwa ngumu lakini wameonyesha Simba ni timu kubwa,” amesema Gomes.

Gomes amesema amewapumzisha baadhi ya nyota sababu kuelekea mchezo wa mwisho wa ligi ambao tutakabidhiwa taji la ubingwa tunahitaji kupata ushindi ili tusherehekee vizuri.

“Jumapili tuna mechi dhidi ya Namungo ambayo tutakabidhiwa taji hivyo tunahitaji kushinda ili sherehe za ubingwa zifane ndiyo sababu ya kuwapumzisha baadhi ya nyota,” amesema Gomes.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER