Mlinzi wa kushoto, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ leo atakiongoza kikosi cha Simba Queens katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifier 2021 dhidi ya Lady Doves utakaopigwa Uwanja wa Kasarani saa saba mchana.
Fetty anavaa kitambaa cha unahodha kutokana na Violeth Nicholaus kupata majeruhi katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Vihiga na ambapo ataukosa mchezo wa leo.
Mlinda mlango Gelwa Yona ameanza katika mchezo wa leo akichukua nafasi ya Zubeda Mgunda ambaye yupo benchi.
Kama kawaida safu ya ushambuliaji itaongozwa na Oppah Clement na Mawete Musolo ambao wameonyesha uwezo mkubwa ingawa hatukupata nafasi ya kutinga fainali.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
- Gelwa Yona
- Maimuna Hamis
- Dotto Evarist
- Fatuma Issa ©
- Julietha Singano
- Danai Bhobho
- Asha Djaffar
- Joelle Bukuru
- Oppa Clement
10.Mawete Musollo - Aisha Juma
Wachezaji wa Akiba
- Zubeda Mgunda
- Janeth Shija
- Shelda Boniface
- Ruth Kipoyi
- Silivia Thomas
- Koku Kipanga
- Zena Khamis
- Violeth Thadeo
- Wema Richard