Fadlu: Tupo tayari kwa ajili ya Pamba Jiji Kesho

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji yamekamilika na wachezaji wapo tayari kuhakikisha pointi tatu zinapatikana.

Kocha Fadlu amesema jana wachezaji wamefanya mazoezi na leo jioni watafanya pia katika Uwanja wa CCM Kirumba na malengo yetu ni kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu ugenini.

Akizungumzia kuhusu nyota waliokuwa kwenye majukumu ya timu za taifa kocha Fadlu amesema haitakuwa na athari kubwa kwenye maandalizi ya mchezo hasa kwakuwa wengi wamepata nafasi ya kucheza na pia walikuwa nyumbani.

“Mechi za ugenini zimekuwa na ugumu kuliko za nyumbani na hii inatokana na uwanja ingawa tumejiandaa kuhakikisha tunapambana ili kupata pointi zote tatu.”

“Ratiba ya mechi za Kalenda ya FIFA haijaharibu maandalizi kuelekea mchezo wetu wa kesho, wachezaji wengi wametumika kwenye timu zao za Taifa hivyo wapo timamu kimwili na wapo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Pamba,” amesema Kocha Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia Shomari Kapombe amesema wao kama wachezaji wapo tayari kuhakikisha wanapambana hadi mwisho na kufuata maelekezo ya mwalimu ili kuwapa furaha Wanasimba.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunafahamu Wanasimba wanahitaji furaha nasi tupo hapa kuhakikisha tunakamilisha furaha yao,” amesema Kapombe

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER