Fadlu, Mukwala wang’ara tuzo za NBCPL Mwezi Mei

Kocha Mkuu Fadlu Davids amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Mei.

Fadlu amewapiku Miloud Hamdi wa Yanga na Rachid Toussi wa Azam FC ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Fadlu ametuwezesha kushinda mechi zote tano tulizocheza mwezi Mei ambao ni dhidi ya Tanzania Prisons, Mashujaa, Pamba Jiji, KMC na Singida Black Stars.

Hii ni mara ya tatu kwa Fadlu kupata tuzo ya Kocha bora wa mwezi baada ya kufanya hivyo mwezi Machi na Agosti.

Nae mshambuliaji, Steven Mukwala amechaguliwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC wa mwezi Mei kutokana na kiwango bora alichokionyesha na mchango mkubwa kwa timu.

Mukwala amewapiku kiungo wetu mshambuliaji, Jean Charles Ahoua na mshambuliaji wa Mashujaa, Jaffar Kibaya alioingia nao fainali.

Katika kipindi cha Mwezi Mei Mukwala amecheza mechi nne sawa na dakika 233 akifunga mabao matatu na kusaidia kupatikana kwa jingine moja.

Hii ni mara ya pili kwa Mukwala kutwaa tuzo hiyo baada ya kufanya hivyo mwezi Machi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER