Kocha Mkuu Fadlu Davids amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC wa mwezi Machi baada ya kuwapiku Rachid Toussi wa Azam FC na David Ouma wa Singida Black Stars aliokuwa ameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Katika mwezi Machi Fadlu ametuongoza kwenye mechi mbili dhidi ya Dodoma Jiji tulioibuka na ushindi wa mabao 6-0 na Coastal Union tulioishinda mabao 3-0.
Kwa upande wake mshambuliaji Steven Mukwala amewapiku kiungo wetu Elie Mpanzu na mlinzi wa kushoto wa Azam Pascal Msindo aliyekuwa kaingia nao fainali.
Katika mwezi huo Mukwala amefunga mabao manne ikiwemo hat trick aliyofunga dhidi ya Coastal Union.