Fadlu: Kilimanjaro Wonders wametupa changamoto

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema licha ya ushindi mnono wa mabao 6-0 tuliopata dhidi ya Kilimanjaro Wonders katika mchezo wa hatua ya 64 ya CRDB Federation Cup lakini kikosi hicho kimetupa changamoto kubwa uwanjani.

Fadlu amelipongeza benchi la ufundi la timu hiyo pamoja na wachezaji kwa kazi kubwa waliyofanya ingawa tuliwazidi hadhi pamoja na uzoefu wa mashindano.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko makubwa kwenye kikosi katika mchezo wa leo, Fadlu amesema lengo ni kuhakikisha wachezaji wanapata nafasi kubwa ya kucheza kwakuwa tupo mzunguko wa pili na mechi ni nyingi zilizo mbele yetu.

“Ukimtoa Aishi Manula ambaye anasumbuliwa na mafua wachezaji wengine wote wapo fiti, mabadiliko ya mchezo wa leo yametokana na kutaka kuwapa nafasi wachezaji wengine kwakuwa tunafahamu ratiba itakuwa ngumu siku za usoni,” amesema Fadlu.

Aidha Fadlu amewasifia wachezaji kwa kuonyesha kiwango safi huku wengi wao wakiwa hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER