Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema pamoja na umuhimu mkubwa uliopo wa kutafuta alama tatu katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine lakini hatua presha.
Kocha Fadlu amesema itakuwa mechi ngumu kwakuwa kila moja inahitaji pointi ili kujihakikisha kuongoza kundi lakini hatuna presha na tumejipanga kucheza soka safi la kuburudisha.
Akizungumzia hali ya kikosi Fadlu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu na kila mmoja yupo tayari kupambana kuhakikisha tunawapa furaha Wanasimba.
“Haiwezi kuwa mechi rahisi kwakuwa tunahitaji kushinda ili kuongoza kundi na wenzetu wanahitaji hata alama moja lakini hatuna presha tutacheza soka letu tulilolizoea.” amesema Fadlu.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema wapo tayari kuhakikisha tunapata ushindi na kuongoza kundi ili kuwaburudisha Wanasimba.
Awesu amezungumzia pia kuhusu kukosekana kwa mashabiki kuwa wachezaji wameumia lakini kupitia dua na maombi mbalimbali wanaamini wataweza kushinda na kupata pointi tatu na kuongoza kundi.
“Sisi tupo tayari na tunajua kwetu ni kama fainali kwakuwa tunahitaji ushindi ili kuongoza kundi na uwezo huo tunao. Tunahitaji sala na maombi kutoka kwa mashabiki wetu,” amesema Awesu.