Fadlu, Ahoua wang’ara tuzo ya NBC mwezi Agosti

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC wa mwezi wa Agosti.

Fadlu amewapiku, Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Mohamed Abdallah wa Mashujaa ambao aliingia nao kwenye kinyang’anyiro.

Katika mwezi Agosti, kocha Fadlu ametuwezesha kupata pointi sita huku tukifunga mabao saba kwenye mechi mbili tulizocheza.

Kwa upande wake kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua amechaguliwa mchezaji bora baada ya kufunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu (Assist’) katika mechi mbili tulizocheza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER