Emirate, Simba zatoa msaada Kituo cha Watoto Yatima Magomeni

Wadhamini wetu Emirate Aluminium ACP imetembelea na kutoa misaada mbalimbali kwa kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Umra kilichopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam.

Emirate imetoa misaada mbalimbali kama unga, mchele, sukari, unga wa ngano, mafuta ya kula, maharage, chumvi, sabuni, taulo za kike, maji ya kunywa na juisi.

Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amewawashukuru Emirate kwa kutoa kwa jamii katika kipindi hiki cha Wiki ya Simba tunaamini hizi ni baraka kwa Mwenyezi Mungu na zitatusaidia kufikia malengo tuliyojiwekea.

“Ili tuwe ‘unstoppable’ kweli lazima tupate baraka za Mwenyezi na watu wengi watuombee dua na hili linatufanya tuwe karibu na Jamii,” amesema Barabara.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Emirate Aluminium ACP, Issa Maeda amesema wameamua kuungana na klabu kuchangia kwa jamii katika Wiki ya Simba kuelekea kilele cha Tamasha letu la Simba Day litakalofanyika Jumatatu Agosti 8, mwaka huu.

“Sisi kama Emirate tumekuja hapa kuungana na Simba kuchangia chochote kuelekea Simba Day. Tumeona nasi sherehe zetu zifanyike hapa kuwasaidia wadogo zetu katika mahitaji yao ya kimsingi,” amesema Maeda.

Aidha, muasisi wa kituo hicho, Rahma Juma amewashukuru Emirate kwa kushirikiana na Klabu ya Simba kwa msaada huo ambao utawasaidia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji yao ya kibinaadamu huku akituombea mafanikio kwa Mwenyezi Mungu.

“Kituo chetu kina watoto 120 ambao wanasoma, shule za msingi, sekondari, chuo kikuu na wengine vyuo vya kati wakisomea fani mbalimbali kwavhiyo mahitaji yetu ni makubwa na hiki mlichokifanya ni kikubwa, tunawaombea kila lenye kheri pia tunaziomba taasisi nyingine zifanye kama mlivyofanya ninyi,” amesema Rahma.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER