Kampuni ya Emirate Aluminium Profile, imemkabidhi kitita cha Sh 1,000,000 kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison baada ya kuchaguliwa mchezaji bora mashabiki wa mwezi Juni (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).
Emirate Aluminium Profile ndiyo wadhamini wa tuzo hii ambayo walianza kuitoa kuanzia Februari mwaka huu.
Morrison raia wa Ghana amewashinda nyota wawili Nahodha John Bocco na Luis Miqiussone ambao ameingia nao fainali ya kinyan’ganyiro hicho.
Mashabiki ndiyo wenye dhamana ya kupiga kura kupitia tovuti hii rasmi ya klabu baada ya Kamati Maalumu kuchuja majina matatu kutoka matano ya awali yaliyopendekezwa.
Baada ya kutwaa tuzo hiyo, Morrison ameishukuru Emirate Aluminum kwa kudhamini na kuwafanya wachezaji kupambana kwa ajili ya kuisaidia timu.
“Nashukuru kwa kupata tuzo hii kwangu ni jambo kubwa, nimepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzangu hadi kufika hapa. Nawashukuru pia Emirate kwa kutoa tuzo hii ambayo inaongeza hamasa kwetu wachezaji,” amesema Morrison.
Mchanganuo wa kura
Idadi ya kura zilizopigwa 9,356
Morrison amepata kura 6,697 sawa na asilimia 72, Luis kura 1,978 sawa na asilimia 21 huku Bocco akipata kura 681 sawa na asilimia saba.
One Response
Inapendeza wadhamini wetu Morrison amestahili