Duchu: Kambi ya Misri inatujenga

Mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesema kambi yetu ya maandalizi inayoendelea nchini Misri inazidi kuwamairisha kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25.

Duchu amesema wachezaji wote wanapambana ili kujiweka sawa ili msimu utakapoanza wawe tayari.

Dunchu ameongeza kuwa ushindani wa namba umekuwa mkubwa kutokana na ubora wa wachezaji wapya waliosajiliwa pamoja na wenyeji.

Akizungumzia kuhusu benchi la ufundi Duchu amesema “ni wiki moja tu imepita tangu tulivyoanza mazoezi lakini makocha wetu wameonyesha wana vitu vingi ambavyo wanatuongezea.”

“Program za mazoezi ni nzuri, makocha wanatupa mbinu mbalimbali ambazo naamini tukimaliza kambi hapa Misri tutakuwa tayari kwa mapambano,” amesema Duchu.

Duchu pia ametuma ujumbe kwa mashabiki ambapo amesema “tunawaomba mashabiki wetu kuendelee kutusapoti, ili kufikia malengo tuliyojiwekea.

Msimu ujao tumejipanga vilivyo lakini tunahitaji mshikamano kuanzia Uongozi, benchi la ufundi, wachezaji mpaka mashabiki,” amesema Duchu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER