Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC ‘Mzima Dabi’ uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Djibril Sillah aliipatia Azam bao la kwanza dakika ya kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Iddi Nado.
Mlinzi wa kati Che Fondoh Malone alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupatama maumivu dakika ya 20 nafasi yake ikachukuliwa na Chamou Karaboue.
Elie Mpanzu alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 25 baada ya kazi safi iliyofanywa na Kibu Denis aliyetoka na mpira nyuma na kuwazidi kasi walinzi wa Azam na kutoka pasi ya upendo.
Mlinzi wa kati Abdulrazack Hamza alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika 76 baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Zidane Sereri aliisawazishia Azam bao hilo dakika ya 88 baada ya kumalizia mpira mrefu uliopigwa kutoka katikati ya uwanja na Feisal Salum.
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 90+2′) Che Malone (Chamou 20′), Hamza, Kagoma (Mukwala 90+2′), Kibu, Ngoma, Ateba, Ahoua, Mpanzu
Walioonyeshwa kadi:
X1: Mustafa, Mwaikenda, Msindo (Chilambo 87′) Yoro, Fuentes, Zayd (Meza 79′) Syllah, Akaminko, Saadun (Sopu 87′), Feisal, Nado (Sereri 79′)
Walioonyeshwa kadi: Fuentes 45+2′ Yoro 53′