Chasambi: Msimu ujao tutafanya vizuri

Kiungo mshambuliaji, Ladaki Chasambi amesema ana matumaini msimu ujao tutafanya vizuri kutokana na maandalizi na kikosi tulichonacho.

Chasambi amesema kikosi chetu kimeundwa na wachezaji wengi vijana na wapo tayari kuipambania timu kuhakikisha tunafanya vizuri.

Chasambi ameongeza kuwa maandalizi wanayofanya kupitia benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids ni mazuri na hayo yanampa matumaini kuwa msimu ujao tutakuwa bora zaidi.

“Kambi yetu ni nzuri hapa Misri, tunafanya mazoezi chini ya Kocha Fadlu na wasaidizi wake na kila kitu kinaenda sawa na tunaamini tutakuwa bora zaidi msimu ujao.”

“Timu yetu inaundwa na wachezaji vijana na tuna ari ya kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuirejesha Simba katika nafasi yake iliyokuwepo,” amesema Chasambi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER