Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Chama amewashinda Nahodha John Bocco na mlinzi Shomari Kapombe ambao alikuwa ameingia nao fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.
Katika mwezi Desemba, Chama amecheza dakika 540 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine saba.
Mchanganuo wa kura ulivyokuwa
Kura Asilimia
Chama 1829 54.52
Bocco 1415 42.18
Kapombe 111 3.31
Kwa kuibuka mshindi Chama atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.